Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Tanzania ni moja ya nchi ambayo teknolojia ya mawasiliano inakuja kwa kasi sana duniani. Takwimu zinaonesha watu karibu milioni arobaini na tatu wanamiliki simu za mkononi. Hii ni fursa nzuri kwa taasisi za serikali na wadau kuitumia katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii ikiwemo kuyafikia masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Mobile Kilimo (M-Kilimo) ni teknolojia ya kutumia simu ambayo imelenga kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kuyafikia masoko ya mazao yao kwa njia ya simu zao za mkononi. Hii itawafanya waweze kuyafikia masoko hasa hasa wanunuzi wa bidhaa na mazao yao ya kilimo pasipo kupitia adha ya kuyasafirisha mazao hayo kwenda masokoni.

Hivyo, kupitia teknolojia hii wakulima, wafugaji na wavuvi wataweza kutoa taarifa za mazao, bei ya mazao na mahali walipo ili wanunuzi waweze kuwafikia kwa urahisi zaidi. Hii itafungua na kuwakutanisha wauzaji na wanunuzi wengi nchini na kupunguza gharama za kupata taarifa za upatikanaji wa bidhaa za kilimo.

Mobile Kilimo kwa sasa inatoa maelezo hayo na maelezo ya jumla kuhusu kilimo kwa teknolojia ya simu- Asante kwa maendeleo ya kiteknolojia, wakulima, wafugaji, na wavuvi watafaidikika sana na huduma ya Mobile Kilimo.

Kutumia huduma hii ya M-Kilimo


PIGA *152*00#


Chagua namba 7. Kilimo, Ufugaji


Kisha fuata maelekezo

Unakaribishwa kujiunga na huduma ya habari za kilimo, ufugaji na uvuvi.