Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA KITALU CHA WILAYA YA IGUNGA KUPATA ELIMU YA UDHIBITI WA VISUMBUFU

Richard Mtamani

29th January, 2022 12:31
Wakulima wa Zao la Pamba Kitalu cha Wilaya ya Igunga  kupata Elimu ya Udhibiti wa Visumbufu

Pamba ni zao la kimkakati ambalo limeendelea kunufaisha wakulima wengi Wilayani Igunga. katika msimu wa kilimo 2021/2022  wakulima wameendelea kutunza zao la Pamba katika Hatua mbalimbali. wengi wao walipanda zao hilo mwezi Novemba na kurudia mwezi disemba kutokana na kuchelewa kwa mvua. hata hivyo wakulima wanathibitisha hali nzuri ya Pamba mashambani katika ukuaji japo tayari wataalamu wametembelea mashamba hayo na kubaini mashambulizi makubwa ya Aphids na Jassids katika maeneo yote yenye Pamba zilipandwa hadi disemba 2021. picha hapo juu zinaonyesha hali ya mashambili kutoka kwenye shamba la Mkulima Makala Shija wa Kijiji cha Mangungu, Kata ya Bukoko, Wilaya ya Igunga.

Maafisa Ugani wa maeneno tofauti ya Wilaya ya igunga wameendelea kushauri wakulima kuanza kupulizia viwatilifu vinavyopatikana ofisi za vyama vya msingi katika vijiji vyao ili kukabiliana na uharibifu huo wa wadudu kwenye zao la Pamba. Mimi Richard Mtamani, Afisa Kilimo Kata ya  Bukoko.


Mirejesho